Picha kwa hisani –
Huduma za afya katika hospitali za serikali humu nchini zimetatizika baada ya wahudumu wa afya kuanza mgomo wao hii leo.
Muungano wa wahudumu wa afya nchini KMPDU hapo jana ulihairisha mgomo huo kwa siku 14, ili kutoa nafasi zaidi ya mazungumzo na baraza la kitaifa la ushauri nchini.
Hata hivyo wahudumu wa afya katika baadhi ya hospitali wamesema kwamaba wataendelea na mgomo huo hadi pale serikali itakapo shughulikia matakwa yao.
Gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Kingi aidha amesema kwamba huduma za matibabu zinaendelea kama kawaida katika kaunti hiyo ya Kilifi.
Wahudumu hao wanalalamikia mazingira duni ya kufanya kazi, vyombo vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona, kucheleweshwa kwa mishahara yao miongoni mwa matakwa mengine.