Story by Ali Chete-
Mgomo wa wahudumu wa afya kaunti ya Mombasa umeratibiwa kuanza rasmi siku ya Jumatatu iwapo serikali ya kaunti hiyo haitatimiza matakwa ya wahudumu hao.
Mgomo huo utajumuisha vitengo vyote vya wahudumu wa afya wakiwemo madaktari, wauguzi, maafisa wa maabara, maafisa wa kliniki, maafisa wa huduma za utoaji dawa miongoni mwa wengine.
Mwenyekiti wa Muungano wa madaktari nchini KMPDU kanda ya Pwani Dkt Ahmed Hassan Mkuche amesema serikali ya kaunti ya Mombasa imeshindwa kutekeleza matakwa ya wahudumu hao ikiwemo kutowalipa mishahara yao vyema
Dkt Mkuche amesema tayari wamewasilisha kesi Mahakamani ili kuishinikiza serikali ya kaunti ya Mombasa kuhakikisha inawajibikia majukumu yake huku akidai kwamba wahudumu wa afya kuanzia siku ya Jumatatu wataanza rasmi mgomo wao.
Kwa upande wake Katibu mkuu wa Muungano wa maafisa wa huduma za utaoji dawa Juma Abdallah Ali amesema wahudumu hao hawatarudi kazini iwapo serikali ya kaunti hiyo haitawajibikia majuku yake.