Story by Ali Chete –
Wahudumu wa Afya katika kaunti ya Mombasa wamesisitiza kwamba hawatarudi kazini hadi pale matakwa yao yatakapotekelezwa.
Katibu wa maafisa wa Kliniki katika kaunti hiyo Frankline Makanga amesema makataa waliyoyatoa kwa serikali ya kaunti hiyo yamekosa kuangaziwa huku akishikilia kwamba huduma za afya katika hospitali na zahanati za umma zitasambaratishwa.
Makanga amesema kwa sasa wahudumu hao hajawalipwa mishahara yao kwa muda wa miezi miwili sawa na kutolipiwa bima ya afya hatua ambayo imechangia wengi wao kupitia hali ngumu.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Wanamaabara katika kaunti hiyo Moses Maingi amewataka viongozi kukoma kuingiza siasa katika swala hilo sawa na kutowatishia kwamba watafutwa kazi.
Kauli zao zimeungwa mkono na Emily Musoi aliyesema hawatalegeza kamba katika swala hilo hadi pale serikali ya kaunti hiyo itakaposhughulikia matakwa hayo.