Story by Ali Chete-
Wahudumu wa Afya katika kaunti ya Mombasa wametishia kushiriki mgomo iwapo serikali ya kaunti hiyo itaendelea kuchelewesha mishahara yao ya mwezi Januari na Februari.
Katibu mkuu wa Muungano wa madaktari nchini KMPDU tawi la Pwani Dkt Nassir Shaban imesema serikali ya kaunti ya Mombasa haijalipa wahudumu hao mishahara yao ya miezi miwili licha ya serikali ya kaunti hiyo kupokea mgao wa fedha kutoka kwa serikali kuu.
Katibu mkuu wa Muungano wa maabara kaunti ya Mombasa Moses Kiteme amesema viongozi wa kaunti hiyo wamezama katika siasa za kujipigia debe na kusahau maslahi ya wafanyikazi hao.