Picha kwa hisani –
Wahudumu wa afya katika Bandari ya Mombasa wamejiunga na wenzao wa maeneo ya mpakani na hospitali nyingine za umma katika Kaunti ya Mombasa katika mgomo unaoendelea.
Wakiongozwa na Dennis Mwasi, wahudumu hao wa Serikali ya kitaifa wamesema wamepuuzwa na kuendelea kufanya kazi katika mazingira magumu.
Kulingana na Mwasi, licha ya kuwa katika hatari ya maambukizi ya virusi vya corona wahudumu hao wamekosa vifaa vya kujikinga na virusi hivyo.
Wakati uo huo Mwasi ametaka kuajiriwe wahudumu zaidi wa afya katika sekta muhimu za umma ikiwemo katika bandari ya Mombasa na maeneo ya mpakani ili kuzuia mizigo iliyo na hatari za kiafya kupenya nchini.