Picha kwa Hisani –
Wizara ya Afya nchni imedokeza kuwa tangu kisa cha kwanza cha maambukizi ya virusi vya Corona kuripotiwa nchnim ni wauuguzi 945 pekee walioambukizwa Corona.
Akitangaza takwimu hizi, Katibu mkuu msimamizi katika Wizara hiyo Dkt Mercy Mwangangi amesema kufikia sasa ni wahudumu 16 pekee waliopoteza maisha kutokana ugonjwa wa Corona kutoka kwa kaunti 35.
Hata hivyo Dkt Mwangangi amesema katika mda wa saa 24 zilizopita, watu 183 wamethibitishwa kupata maambukizi hayo kutokana na sampuli 4,188 na kupelekea idadi hiyo kufikia watu 36,576.
Dkt Mwangangi amesema kati ya watu hao 183, wagonjwa 14 ni raia wa kigeni, wengine wakiwa wakenya huku wanaume wakiwa 131 na wanawake wakiwa 52 huku mtoto wa miezi minane ni kati ya walioambukizwa virusi hivyo.
Wakati uo huo amesema watu 82 waliokuwa wakiugua Corona wamethibitishwa kupona na kupelekea idadi ya waliopona kufikia watu 23,611 huku watu watano wakiripotiwa kuaga dunia na idadi hiyo kufikia watu 642.