Picha kwa hisani –
Shirika la sauti ya wazee limewalaumu baadhi ya wahubiri wanaombea wanajamii katika kaunti ya Kilifi,kwa madai kwamba wamechangia ongezeko la visa vya mauji ya wazee kwa tuhuma za uchawi.
Katibu wa shirika hilo Simon Mvondi amesema wahubiri wanaofungua makanisa bila vibali kutoka kwa serikali wamechangia uhasama huo,akitaka makanisa yote kuchunguzwa na yale yasio na vibali yafungwe mara moja.
Mvondi amesema mauaji hayo yamekithiri katika maeneo ya Ganze,Magarini na Malindi,akisema baadhi ya viongozi wa serikali na wa kitamaduni wanahusika katika kutoa vibali vya kuwawezesha washukiwa wa mauaji hayo kukwepa mkono wa sheria.