Wasanii Wahu na Size 8 wameachilia kolabo kwa jina Power Power.
wimbo huu ni wa kwanza kufanywa na wasanii hao tangu walipokiri kuwa Yesu ni Bwana.
Wimbo huu unajiri siku chache tu baada ya msanii Size 8 ambaye jina lake rasmi ni Linet Masiro kufichua makubwa kuhusu hali yake ya kiafya baada ya kujifungua mtoto wake wa kwanza akiwa na Dj Mo.
Wahu amabye enzi zake alitesa na kibao Still a Liar anasemekana kuvaa msalaba baada ya mumewe David Mathenge maarufu kama Nameless kuokoka kifo pale alipopasuka mishipa ya kichwa.