Picha kwa hisani –
Serikali kupitia idara ya upelelezi wa jinai DCI, imefungua upya kesi kuhusu dhulma walizotendewa wahanga wa gasia za baada ya uchaguzi za mwaka 2007/2008 ili kuhakikisha wanapata haki.
Akihutubia waathiriwa hao katika makao makuu ya idara ya DCI,mkurugenzi wa idara hio George Kinoti amesema wamenakili kesi 72 za mauaji,kesi 44 za watu kufukuzwa katika ardhi zao na kesi 118 za vitisho kwa waathiriwa hao.
Kinoti amesema wahanga wa gasia za baada ya uchaguzi wako huru kuandikisha taarifa kwa idara hio,na kwamba serikali imeidhinisha zoezi hilo baada ya waathiriwa hao kupiga ripoti kwamba wameanza kupokea upya vitisho.
Kinoti hata hivyo amewataka waathiriwa wa gasia za baada ya uchaguzi wanaoendelea kupokea vitisho kutokua na hofu,kwani vitengo mbali mbali vya polisi vitahakikisha wanalindwa.