Wakaazi katika eneo la Malindi kaunti ya kilifi wamenufaika na huduma za bure za matibabu ya upasuaji kwa maradhi mbali mbali yanayowakabili.
Akiongea na wanahabari katika hospitali ya malindi wakati wa zoezi hilo lililofadhiliwa na serikali ya kaunti ya kilifi na shirika la Wound Care Society of Kenya, Daktari Nangole wanjala amesema umaskini miongoni mwa wakaazi eneo hilo umepelekea wengi wao kushindwa kugharamia huduma za upasuaji kwa maradhi yanayowakumba.
Daktari Wanjala ambaye ni mhadhiri mkuu wa kitengo cha upasuaji katika chuo kikuu cha Nairobi amesema kuwa serikali inapaswa kuwekeza zaidi katika kuongeza idadi ya madaktari wa upasuaji nchini.
Kwa upande wake afisa mkuu msimamizi wa hospitali ya kaunti ndogo ya Malindi Evans Ogeto amesema kuwa zaidi ya wakazi 100 wenye magonjwa mbali mbali yanayohitaji upasuaji watahudumiwa.