Story by Gabriel Mwaganjoni-
Wagonjwa wa kisukari katika kaunti ya Mombasa wamelalamikia hali ngumu katika kupata dawa na misaada mingine ikiwemo ya lishe inayostahili kufuatia changamoto za kimaisha.
Kulingana na kundi la Diabuddies linalongozwa na Linet Mavu hali imekuwa ngumu huku idadi ya wagonjwa wa kisukari wasiyoweza kumudu gharama za matibabu ikiongezeka kila uchao.
Mavu amesema kwamba changamoto hizo za kimaisha zimepelekea ongezeko la changamoto za kiafya kwa wagonjwa hao.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa, Mavu ameomba msaada kwa kundi hilo kwani ina walazimu wagonjwa wa kisukari kuungana na kuchangiana fedha chache ili kuwawezesha kumudu dawa na lishe maalum.