Wafungwa watatu katika gereza la wanaume la Kwale ni miongoni mwa watahiniwa watakao fanya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE.
Akiongea na wanahabari afisa msaidizi katika gereza hilo Stanely Mbaji amesema kuwa wafungwa wengine wawili waliosajiliwa kufanya mtihani huo mwaka huu hawajulikani waliko hasa baada ya kukamilisha vifungo vyao.
Mbaji aidha amesema kuwa mikakati imeekwa kukabili visa vya udanganyifu wakati wa mtihani huo sawa na kuhakikisha kuna usalama wa kutosha.
Watahiniwa hao wanaotumikia kifungo cha miaka mitano katika gereza hilo wameeleza matumaini yao kwamba watafanya vyema kwenye mtihani huo huku wakiwataka wafadhili kujitokeza kusimamia masomo yao ya shule ya upili.
Taarifa na Mariam Gao.