Story by Taalia Kwekwe-
Mamlaka ya mazingira nchini NEMA imetoa makataa ya siku 14 kwa wale wanaoendeleza shughuli za uchimbaji mawe na mchanga katika kijiji cha Kilole eneo la Kinondo gatuzi dogo la Msambweni kaunti ya Kwale kuzingatia sheria zilizowekwa na serikali.
Mkurugenzi wa mamlaka hiyo kaunti ya Kwale Godfrey Wafula, amesema baada ya siku 14 kukamilika,watafanya oparesheni kali kwa kushirikiana na vitengo mbali mbali vya serikali na wale wasiozingatia sheria watanaswa.
Akizungumza wakati wa kikao cha kuhamasisha wakaazi kuhusu sheria za timbo za mchanga, mawe na madini, Wafula amesema ni lazima wale wanaojihusisha na uchimbaji mchanga na mawe wapate cheti maalum kutoka kwa mamlaka hiyo.
Wakati uo huo Wafula ametoa hamasisho kwa jamii kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira.