Wafanyikazi wanane wa Radio Kaya wanauguza majeraha madogo baada ya gari walilokua wameabiri kuhusika katika ajali ya barabarani katika eneo la bixa huko tiwi barabara kuu ya Likoni – Lungalunga.
Kulingana na walioshuhudia ajali hio wamesema ajali hio imetokea baada ya gari waliokua wakisafiria kugongana na lori la kubeba magodoro hali iliopelekea wanane hao kujeruhiwa.
Madakatari wanaowahudumia katika hospitali ya diani huko ukunda wamethibitisha kuwa wanane hao wako katika hali nzuri ya kiafya na kwamba wataruhusiwa kuondoka hospitali punde tu watakapomaliza kutibiwa.
Miongoni mwa waliohusika katika ajali hio ni pamoja na Beatrice dama kahindi,kalambua,Robby Dallaz ,Rasi Mangale ,Chikoyokoyo,Caroline Mkamburi Suleiman Mwajenjewa na Hassan Nyawa ambae ni dereva wa kituo hiki.