Shughuli za kawaida zimetatizika mjini Malindi baada ya wafanyikazi wa idara ya mazingira kaunti ya Kilifi walioachishwa kazi siku chache zilizopita kuandamana.
Waandamanaji hao waliokua wamebeba taka na kuzitawanya katika maeneo mbali mbali ya mji wa Malindi, wamekashifu hatua ya serikali ya kaunti ya Kilifi ya kuwafuta kazi bila notisi ,wakidai kwamba haki zao zimekiukwa.
Imelazimu maafisa wa polisi kuingilia kati kuwatawanya waandamanaji hao waliokua wakichafua mji huo huku baadhi yao wakitiwa nguvuni.
Kiongozi wa wafanyikazi hao Mramba Mweni amesema kuwa kufikia sasa hawajajua hatma yao kuhusiana na mgogoro unaowakumba.
Kwa upande wake waziri wa mazingira katika serikali ya kaunti ya Kilifi Kiringi Mwachitu amesema kuwa wafanyikazi hao watarejeshwa kazini baada ya majadiliano yanayoendelea kuhusu jinsi watakavyolipwa kukamilika.
Taarifa na Charo Banda.