Picha kwa hisani –
Wafanyibiashara wa Samaki katika Soko la watamu kule kaunti ya Kilifi wanalalamikia kucheleweshwa kufunguliwa kwa Soko la Samaki.
Wafanyibiashara hao wamesema kuendelea kucheleweshwa kwa soko hilo kumeathiri pakubwa kwa biashara zao huku wakiitaka Wizara kuliwajibikia swala hilo.
Wakiongozwa na Mwenyekiti wao Athman Mwambire, wafanyibiashara wanasema ni mwaka wa sita sasa soko la watamu halijafunguliwa, licha ya masoko mengine katika kaunti ya Kilifi kufunguliwa.
Mwambire amesema kufunguliwa kwa soko hilo kutasaidia katika kukusanya na kunakili taarifa muhimu kuhusiana na shughuli za uvuvi katika eneo hilo, sawia na kuimarisha utendakazi wa wavuvi hao.