PICHA KWA HISANI
Idara ya utawala katika kaunti ya Mombasa imeharamisha shughuli za uchuuzi katika pande zote mbili za kivuko cha feri cha Likoni.
Kamishna wa kaunti hiyo Gilbert Kitiyo, amesema wafanyabiashara waliokabidhiwa vibanda maalum pekee katika kivuko hicho ndio watakaoruhusiwa kuendeleza shughuli zao za kibiashara.
Kitiyo, amesema ni lazima wafanyabiashara hao wazingatia maswala ya usafi, kwao na kwa wateja wao la sivyo vibanda hivyo vitafungwa.
Wakati uo huo amewahimiza wafanyibiashara hao kuzingatia maagizo yanayotolewa na serikali kuhusu jinsi ya kujikinga na maambukizi ya Corona.