
Mwenyekiti wa shirika la biashara na viwanda nchini Mustafa Ramadhan. Picha / Sammy Kamande
Mwenyekiti wa shirika la biashara na viwanda nchini Mustafa Ramadhan amewataka wafanyi biashara wachanga kujitolea katika kupata mafunzo ili kujiwezesha katika kuendeleza na kumudu biashara zao.
Akizungumza mjini Mombasa kwenye warsha ya kukabidhiwa kwa ofisi rasmi, Mustafa amesema wanampango wa kuunda video fupi za biashara sawia na kutumia mitandao ili kukuza soko la biashara ndogo ndogo katika kaunti ya Mombasa.
Hata hivyo ametaja kushirikiana na sekta mbali mbali za kibiashara kutoka kaunti hio kutawasaidia pakubwa katika kupiga jeki biashara.
Mustafa pia amesema wanampango wa kuanzisha mafunzo kwa wanabiashara wachanga ili kuwajuza namna za kupambana na changamoto ambazo huwakumba wafanyibiashara wachanga mjini Mombasa.
Taarifa na Sammy Kamande.