Idadi kubwa ya wafanyabiashara wamekwama kwenye vituo vya magari hasa katika miji ya Voi, Mwatate na Wundanyi baada ya kukosa huduma za usafiri.
Wafanyabiashara hao ambao huendeleza shughuli zao siku kwenye soko la Maungu na Msau wanahofia kuandikisha hasara kubwa wakati huu ambapo msako unaendelezwa dhidi ya magari yasiotimiza sheria za michuki ambazo zimeanza kutumika tena leo.
Baadhi wamelazimika kutumia usafiri wa kibinafsi ili kufikisha bidhaa zao sokoni.
Taarifa na Fatuma Rashid.