Story by Janet Shume-
Wafanyabiashara katika soko la Kongowea kaunti ya Mombasa wanalalamikia mazingira mabovu ya kufanyia kazi katika soko hilo hali ambayo imeathiri biashara zao.
Wakiongozwa na Jackson Odhiambo, wafanyabiashara hao wamesema kutokana na kuendelea kushuhudiwa kwa mvua hali ya mazingira katika soko hilo imezidi kuwa mbaya na kupelekea kupungua kwa wateja.
Aidha wameitaka serikali ya kaunti ya Mombasa kukarabati eneo hilo ikiwemo barabara ili kuimarisha biashara katika soko hilo.