Wafanyibiashara katika eneo la Bamburi mwisho wamedai kupata hasara kwa kukosa wateja kufuatia genge la wahalifu lililovamia eneo hilo mapema wiki hii.
Wakiongozwa na Salimu Walalo ambaye anafanya biashara ya kuuza bidhaa dukani katika eneo hilo ametaja kupungua kwa wateja huku akidai wateja wengi wamekosa kufika kufuatia kuhofia usalama wao.
Wakati uo huo wameitaka idara ya usalama kuingilia kati na kuhakikisha usalama unapatikana sawia na kurudisha hali ya kawaida katika eneo hilo.