Picha kwa hisani –
Wadau mbalimbali wa maswala ya maji ikiwemo serikali ya kitaifa, zile za kaunti na wadau wa kimazingira kule kaunti ya Kilifi wameanzisha mchakato wa kutatua tatizo la uhaba wa maji katika kaunti ya Kilifi.
Akizungumza wakati wa halfa ya kimazingira na hatua za kukabili uhaba wa Maji kaunti ya Kilifi, Mkurugenzi wa kampuni ya usambazaji maji ya Malindi Gerald Mwambire amesema kampuni hiyo hulazimika kulipa hadi shilingi milioni 40 kila mwezi kugharamia umeme.
Mwambire amesema gharama hiyo kubwa imechangiwa na malimbikizi ya deni la umeme ambalo huchangia ukosefu wa maji kila mara katika kaunti hiyo.
Kwa upande wake Waziri wa maji katika Serikali ya kaunti ya Kilifi Kiringi Mwachitu amesema takriban shilingi bilioni mbili zimetengwa kuimarisha sekta ya maji na usafi katika kaunti hiyo.