Story by Hussein Mdune –
Wadau wa sekta ya elimu katika kaunti ya Kwale wamedai kwamba eneo la Samburu/Chengoni litaimarika zaidi kielimu iwapo wazazi wataekeza katika elimu.
Wadau hao wakiongozwa na mmiliki wa Shule ya kibinafsi ya Muungano iliyooko eneo la Samburu Hamis Rai Nyondo amesema hatua ya wazazi kutowajibikia majukumu yao imechangia watoto wengi kutofauli kimasomo.
Hamis amesema eneo la Samburu/Chengoni bado linapitia changamoto kutokana na kutopigwa jeki kwa sekta hiyo.
Wakati uo huo amewata wazazi kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu ili kuhakikisha wanafunzi wanafanya vyema masomo.