Story by Ephie Harusi–
Takriban watu elfu 20 wanaoishi karibu na mashamba yanayotumika kuvuna chumvi eneo Magarini kaunti ya Kilifi, wanadaiwa kuathari kiafya kutokana na shughuli za uvunaji chumvi.
Afisa wa mazingira katika shirika la Natural justice kaunti ya Kilifi, Justus Kithi Tsofa amesema huenda idadi ya kubwa ya jamii waliotharika kiafya na shughuli za uvunaji chumvi ikaongezeka.
Akizungumza mjini Malindi, Tsofa amesema tatizo la baadhi ya akina mama kuaribika mimba kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa katika eneo hilo ni mojawapo ya athari za kiafya.
Tsofa amezilaumu kampuni za chumvi katika eneo bunge hilo kwa kuchangia kuathirika kwa shughuli za uvuvi na hata ufugaji wa nyuki kutokana na ukataji miti ya mikoko kiholela.
Mdau huyo wa maswala ya mazingira amesema hatua hiyo imechangiwa na wananchi kutokuwa na ufahamu kuhusiana na haki zao.