Story by Ngombo Jeff
Shirikisho la kitaifa la wakulima la KENAFF pamoja na wadau wengine wa kimazingira wazindua sheria ya asilimia 10 ya upanzi wa miti katika eneo la Gede kaunti ya Kilifi.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa upanzi wa miti iliyofanyika katika shule ya msingi ya Jimba katika eneo hilo, Mwenyekiti wa Shirikisho hilo kaunti ya Kilifi Getrude Bahati amesema kuna haja ya wakulima kuelimishwa kuhusu umuhimu wa sheria hiyo.
Getrude amesema endapo wakulima watazingatia upanzi wa miti basi itawasaidia pakubwa katika kuvutia mvua na sawa na kulinda mazingira.
Kwa upande wake Afisa wa utafiti katika shirika la utafiti wa misitu nchini Kevin Mwema, amesema jumla ya miche 500 imepandwa wakati wa halfa hiyo na itawasaidia wanafunzi kuelewa jinsi ya kuhifadhi mazingira.