Story by Ngombo Jeff-
Wadau wa elimu katika eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi sasa wanaitaka serikali, mashirika ya kijamii na asasi husika za elimu kushirikiana katika kuboresha miundo msingi ya shule za eneo hilo.
Kulingana na Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Mtoroni eneo la Mwendapole kaunti ya Kilifi Josiah Wanje, shule hiyo ina uhaba mkubwa wa madawati sawa na ukosefu wa sakafu madarasani.
Wanje amesema shule hiyo ina idadi ya wanafunzi 540 huku idadi ya madawati katika shule hiyo ikiwa ni 40 pekee.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa shule hiyo Patrick Chirongo, amesema ukosefu wa madawati shuleni humo umechangia wanafunzi wengi kutohudhuria masomo vyema.