Story by Mercy Tumaini:
Idara ya elimu katika eneo bunge la Kaloleni kaunti ya Kilifi imedokeza kwamba eneo bunge hilo linaongoza kwa idadi ya watoto ambao hawahudhuri masomo.
Mkurungezi wa elimu katika eneo hilo Josphine Lomata amesema jumla ya watoto 2,900 walio na umri kati ya miaka 6 na 13 kutoka eneo bunge hilo hawajapelekwa shule.
Josphine amesema kwa ushirikiano na mashirika mengine ikiwemo Shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, wameanzisha mapango wa kuwahamasisha wazazi wa eneo hilo kuhusu umuhimu wa kuwapeleka watoto wao shule.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo afisa mkuu mtendaji wa tume ya kuajiri walimu nchini TSC Nancy Macharia, amesema serikali itaendeleza mpango huo ili kuhakikisha watoto wote walio na umri wa kwenda shule kutoka eneo hilo wanapelekwa shule.