Story by Rasi & Chiro-
Mkurungenzi wa elimu katika kaunti ya Kwale Martin Cheruiyot amesema viwango vya elimu katika kaunti hiyo vimeimarika zaidi.
Akizungumza na Wanahabari wakati wa siku ya elimu katika bustani ya Baraza mjini Kwale, Cheruiyot amesema hali hiyo imechangiwa na mikakati mwafaka iliyowekwa na serikali pamoja na wadau wa elimu.
Cheruiyot amehoji kwamba japo kumekuwa na changamoto za baadhi ya wanafunzi kutojiunga na shule za upili kwa wakati kutokana na ukosefu wa mahitaji ya msingi, idadi hiyo ni kidogo mno na juhudi hizo zimeboreshwa.
Wakati huo uo amewataka wazazi kuwajibikia majukumu yao vyema na wala sio kusubiri hadi washinikizwe na serikali wakati wanafunzi wanapomaliza darasa la nane.
Hata hivyo wadau hao wa sekta ya elimu kaunti ya Kwale, wanalenga kujadili jinsi watakavyoboresha viwango bora vya elimu kaunti ya Kwale.