Story by Ali Chete-
Wadau wa maswala ya Amani na usalama katika kaunti ya Mombasa wameendeleza hamasa kwa jamii kuhusu umuhimu wa kudumisha amani wakati huu ambapo taifa linashuhudia mihemko ya kisiasa.
Naibu Kamishna wa gatuzi dogo la Nyali Henry Rop amesema kufuatia vurugu za kisiasa wakati wa kura za mchujo za vyama katika kaunti hiyo wameamua kushirikiana na wadau hao ikiwemo mashirika ya kijamii ili kuhakikisha wanahamasisha wakaazi umuhimu wa amani.
Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Haki Africa Salma Hemed amesema tayari mikakati mwafaka imeidhinishwa ili kuhakikisha usalama unadumishwa.
Kauli zao zimeungwa mkono na Mkurugenzi mkuu wa shirika la Nyali Justice Center Christine Khabuya aliyesema ushirikiano huo utahakikisha jamii inadumisha amani.