Wadau wa afya kaunti ya Kwale wamekiri Kwamba kaunti hio imenakili idadi ya juu ya visa vya mimba za utotoni na kwamba huenda takwimu zilizotolewa hivi majuzi kuhusu visa hivyo viko sahihi.
Muuguzi msimamizi wa afya katika kaunti hiyo Edward Mumbo amesema tatizo la mimba za utotoni limekuwepo katika kaunti hio kabla ya janga la Corona na visa hivyo huenda vimeongezeka wakati uu huu ambapo watoto wapo nyumbani.
Afisa huyo wa afya kaunti ya Kwale aidha amesema kwa sasa wanafuatilia takwimu hizo ili kubaini maeneo yaliandikisha idadi ya juu ya visa hivyo kabla ya kuidhinisha mikakati ya kumaliza mimba za utotoni.
Hata hivyo kamanda wa polisi kaunti ya Kwale Joseph Nthenge amewahimiza wakaazi wa kaunti hio kuripoti visa vya dhulma zinazotendewa watoto wao ili kukomesha uovu huo.