Story by GAbriel Mwaganjoni-
Wanawake wanaojishughulisha na biashara ya samaki katika eneo la Pwani wamekuwa wakipitia changamoto nyingi ikiwemo kudhulumiwa kingono na wavuvi.
Mwanaharakati wa maswala ya jinsia katika eneo la Kipini gatuzi dogo la Tana delta katika kaunti ya Tana river Habiba Dida amesema kutokana na ukosefu wa vifaa vya wao kujiendeleza katika maswala ya uvuvi wanaume wamekuwa wakiitumia fursa hiyo kuwanyanyasa kimapenzi.
Dida amesema hali hiyo imewakumba wanawake wengi wanaojishughulisha na maswala ya uvuvi na biashara ya Samaki katika kaunti za Mombasa, Kilifi, Kwale, Tana river na Lamu.
Japo wanawake hao wamepokea mafunzo kutoka kwa Shirika la CANCO wanaitaka Serikali kuwaangazia zaidi na kuwapatia vifaa ili wajitegemee katika shughuli zao za uvuvi.