Wachuuzi katika daraja la Liwatoni kaunti ya Mombasa wamelalamikia kufurushwa katika kivuko hicho bila ya kupewa maeneo mbadala ya kuendesha kibiashara.
Mfanyibiashara Fatuma Juma, amesema daraja hilo hutumiwa na watu wa viwango vya chini vya maisha ikilinganishwa na kivuko cha feri cha Likoni ambako sasa hakuna wanunuzi wengi.
Athari hizo zimewakumba baadhi ya wachuuzi wa soko la Marikiti kaunti ya Mombasa, ambao hutegemea kivuko cha feri cha Likoni katika kusafirisha bidhaa zao hadi sokoni humo.
Awali, Mshirikishi mkuu wa Ukanda wa Pwani John Elungata alisema ujenzi wa daraja la Liwatoni umebuni eneo mwafaka la wachuuzi na wachukuzi wa tuk tuk na boda boda kujiendeleza kiuchumi, lakini wachuuzi hao wamekuwa wakipitia changamoto.