Story by Gabriel Mwanganjoni –
Wachuuzi ambao wamekuwa wakiendeleza shughuli zao za kibiashara katika bustani la Mama Ngina wameikosoa Wizara ya utalii nchini kwa kuwazuia kuendeleza shughuli zao katika bustani hiyo.
Wachuuzi hao wamedai kuwa bustani ya Mama Ngina ni eneo lao la kiuchumi na hatua ya kuifunga na kuwatimua wachuuzi hao katika bustani hiyo kumewaathiri kibiashara.
Wachuuzi hao wa vyakula, wale wanaokodisha viti, wapiga picha, wauzaji vinywaji miongoni mwa Wafanyibiashara wengine wametaka kuruhusiwa kuendeleza shughuli zao za uchuuzi ili katika bustani hiyo.
Katika ratba kutoka kwa Wizara ya utalii nchini, bustani hiyo litafunguliwa mwendo wa saa na mbili asubuhi na kufungwa saa tatu asubuhi ili kuwaruhusu watu kufanya mazoezi na kisha kufunguliwa tena saa kumi alasiri hadi saa moja usiku.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini na katibu wa Wizara hiyo Bi Safina Kwekwe, hakuna mikutano ama michezo ya aina yoyote, biashara zitakazoruhusiwa katika bustani hiyo wala watu kuketi au kuegesha magari, baiskeli au hata pikipiki zao.