Viongozi wa kidini kule Malindi kaunti ya Kilifi wametoa makataa ya siku 7 kwa serikali kukabiliana na mhubiri tata Paul Makenzi katika eneo hilo la sivyo wataandamana na kulifunga Kanisa lake.
Wakiongozwa na Kasisi John Leiyo, viongozi hao wamesisitiza kuwa hawatakubali mhubiri huyo wa Kanisa la Good News International kuendelea kuwapotosha wakaazi wa eneo hilo.
Viongozi hao wamedai kuwa mafunzo anayoyatoa mhubiri huyo hayaambatani na jamii huku wakiyataja mafunzo ya mhuburi huyo kama itikadi kali.
Taarifa na Esther Mwagandi.