Picha Kwa Hisani –
Wabunge wa humu nchini wamefanya kikao cha kujadili masuala ya uongozi wa taifa katika hoteli moja jijini Nairobi.
Akizungumza na wanahabari baada ya kikao hicho spika wa bunge la kitaifa Justine Muturi amesemabunge linajukumu la kuwa waangalizi wa utendakazi wa maafisa wa matawi yote matatu ya serikali ikiwemo utendaji,bunge na mahakama.
Kwa upande wake kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa Amos Kimunya ametaka kubuniwa kwa sheria itakayowezesha kuwepo na ushirikiano wa moja kwa moja kati ya bunge la kitaifa na bunge la seneti.
Kimunya ambae pia ni mbunge wa Kipipiri amesema kuna haja ya bunge la kitaifa na lile la seneti kuibuka na mfumo utakaosaidia katika kuzuia ubadhirifu wa fedha za umma unaotekelezwa na maafisa wa serikali.