Baadhi ya wabunge katika kaunti ya Taita Taveta wametaka fedha zilizotengwa na serikali kwa ajali ya kuzikimu familia maskini wakati huu wa janga la Corona fedha hizo kusambazwa hadi mashinani.
Wakiongozwa na Mbunge wa Voi Johnes Mlolwa, wabunge hao wamesema janga la Corona limeathiri wananchi wengi kiuchumi ikiwemo wale wa kaunti ya Taita taveta.
Mlolwa ameitaka serikali ya kaunti hiyo kutenga sehemu maalum ya kuwapima watu virusi vya Corona mjini Voi kwani mji huo unapokea wageni wengi.
Wakati uo huo amewataka wakaazi wa kaunti hiyo kuzingatia masharti yote ya afya ili kujikinga na ugonjwa wa Corona.