Mshirikishi mkuu wa kitengo cha afya kinachoshughulikia virusi vya HIV Kaunti ya Mombasa Zaitun Ahmed amebaini kuwa kati ya waathiriwa 95, 310 wa virusi vya HIV katika kaunti ya Mombasa ni Wathiriwa 43, 773 pekee wanaotumia dawa za kupunguza makali ya maradhi hayo.
Zaitun amesema kuwa kwa idadi hii, waathiriwa 28,520 ni wa kike huku waathiriwa wa kiume wakiwa 14,196.
Hali hii imeashiriwa wazi kwamba asilimia kubwa ya wanaotumia dawa hizo ni wanawake ikilinganishwa na wenzao wa kiume.
Zaitun aidha amefichua kuwa jumla ya watoto 700 wa umri wa kati ya miaka 10 – 14 wanatumia dawa hizo.
Taarifa na Cyrus Ngonyo.