Huku zoezi la kupiga kura likiendelezwa katika vituo mbali mbali katika eneo bunge la msambweni kaunti ya Kwale ,vuta ni kuvute imeshughudiwa katika Kituo cha kupigia kura cha bongwe/gombato.
Hii ni baada ya wafuasi wa mgombea huru wa kiti cha ubunge wa eneo hilo Feisal Bader wakiongozwa na Mbumge wa Nyali Mohamed Ali kudaiwa kukiuka sheria za uchaguzi.
Hata hivyo wafuasi wa mgombea wa ODM Omar Boga wakiongozwa mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharif wametaja purukushani inayoibuliwa na wafuasi wa Feisal kama ishara ya mgombea huyo kushindwa kwenye uchaguzi huo.
Kwa upande wake katibu mkuu wa chama ODM Edwin Sifuna amekashifu tukio hilo akiwataka maafisa wa usalama kuwachukuliwa hatua za kisheria watakaojaribu kuvuruga uchaguzi huo.
Kauli hio imeungwa mkono na mwakilishi wa kike kaunti ya Nairobi Bi Esther Passaries ambaye amewakata wakaazi eneo bunge hilo la msambweni kupiga kura kwa amani.
Hata hivyo waangalizi wa uchaguzi wakiongozwa na Alfaris Bakar kutoka shirika la kutetea haki za binadamu la ELOG wametoa kauli yao juu ya ucgauzi huo.