Vurumai imeshuhudiwa ndani ya ukumbi wa kutatua mizozo ya ardhi katika eneo la Watamu kaunti ya Kilifi uliyoongozwa na Tume ya kitaifa ya ardhi.
Kizazaa kicho kilianza pale Mbunge wa Kilifi Kazkasini Owen Baya kuzua rabsha kutokana na usemi wa Kaimu Mwenyekiti wa Tume hiyo Abigael Mbagaya wa kuwaita wakaazi hao vinyago baada ya wakaazi wawili wa Jimba kukosa kuelewana.
Wakaazi hao wawili wa Jimba walikuwa wakirushiana cheche za maneno kwenye kikao hicho kuhusu umiliki wa kipande cha ardhi ndipo vurumai hilo likaanza.
Ilimlazimu maafisa wa polisi kuingilia katika mzozo huo uliopeleka shuhuli hiyo kusitishwa kwa muda wa saa moja kisha baadaye kuendelea.
Taarifa na Charo Banda.