Wakulima wa mahindi katika eneo la Majaoni mjini Kilifi wanahofu ya kukumbwa na baa la njaa baada ya mahindi yao kushambuliwa na mabuu na kuharibiwa.
Wakulima hao wamesema kuwa wamejaribu kupulizia madawa mabuu hao lakini bado wanaendelea kushambulia mahindi yao.
Japhet Karisa na Hellen Kadzo ambao ni miongoni mwa wakulima hao wamesema kuwa kwa sasa hawatarajii mavuno yoyote kutoka kwa ekari mbili za mahindi ambayo wamekuwa wakitegemea kupata chakula.
Kulingana na Japhet mwaka huu ni wa pili tangu mabuu hao kuzuka na akaitaka serikali ya kaunti kupitia kwa idara ya kilimo kuja na mbegu mbadala ambazo wakulima watapanda badala ya kutegemea kilimo cha mahindi
Taarifa na Marietta Anzazi.