Shirika la kutetea haki za kibnadam la MUHURI limesema kuwa viwango vya elimu katika ukanda wa Pwani kwa sasa vimeimarika sawa na idadi ya wanafunzi wanaojiunga na shule za msingi.
Akiongea mjini Mombasa afisa wa mipango katika shirika hilo, Fredrick Okado amesema kwamba hamasa zinazotolewa na wadau mbali mbali zimechingia watoto wengi katika ukanda wa Pwani kujiunga na shule.
Okado amesema kuwa tamaduni na viwango vya juu vya umaskini miongoni mwa wakaazi wa Pwani umekua kikwazo katika suala la elimu, huku akihimiza wadau wa elimu na mashirika yasiokua ya kiserikali kuvunja tamaduni zilizopitwa na wakati.
Tayari shirika la MUHURI lina mipango ya kuandaa vikao vya kujadili maswala ya elimu katika kila kaunti hapa Pwani ili kutafuta mwelekeo unaostahili katika kukuza viwango vya elimu.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.