Vituo vya televisheni mbali mbali nchini vimetakiwa kuonyesha vipindi ambavyo vimetengenezwa na wakenya.
Kulingana na mmoja wa wazalishaji wa vipindi hivyo Daudi Otieno Anguka amedai vipindi ambavyo wakenya wamekuwa wakivumbua vimepewa asilimia ndogokatika televisheni za humu nchini hali ambayo inalemaza sanaa.
Kwa upande wake mmoja wa wafadhili wa vipaji vya filamu Margaret Mathore amedai kushirikiana na wasanii wachanga wa filamu kumesaidia sana katika kuendeleza maadili ya kiafrika.