Serikali ya kaunti ya Kilifi kupitia bunge la kaunti hiyo imejitokeza na kupinga taarifa kuwa jengo la kifahari la afisi za wawakilishi wadi linalojengwa huko Malindi litagharimu shilingi bilioni moja.
Akiongea na wanahabari katika majengo ya bunge spika wa bunge hilo Jimmy Kahindi amekanusha madai hayo na kumkosoa mbunge wa Kilifi Kazkazini Owen Baya kwa kuendeleza uvumi huo ambao umezua mihemko mikali miongoni mwa wakazi wa Kilifi.
Kulingana na Kahindi mradi huo umetengewa shilingi milioni 408 pekee na wala sio bilioni moja kama ilivyodaiwa.