Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Afrika limehimiza ushirikiano wa jamii, idara ya usalama na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu ili kudhibiti visa vya wazazi kuwadhulumu na kuwanyanyasa watoto wao.
Kulingana na afisa katika kitengo cha dharura katika shirika hilo Mathias Shipeta visa hivyo vimekithiri katika kaunti ya Mombasa na huenda vikaathiri jamii pakubwa.
Shipeta amewahimiza wazazi kuwachunga vyema watoto wao msimu huu wa likizo akisema shirika hilo halitaruhusu wazazi kuendeleza dhulma kwa wanao.
Kauli ya mtetezi huyo wa haki inajiri siku chache baada ya mama mmoja katika eneo la Kisauni kumpiga na kumfungia nyumbani mtoto wake mwenye umri wa miezi sita huku akiendeleza shuighuli zake za kibiashara.
Taarifa na Hussein Mdune.