Taarifa na Kibibi Mwinyihaji
Mombasa, Kenya, Juni 26 – Kamati zinazoshughulika na maswala ya mahakamani kwa wakishirikiana na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu, wameanzisha mchakato wa kujua jinsi watakavyofuatilia kesi za ugaidi na haki kupatikana.
Afisa wa miradi katika Shirika la Search for Common Ground, Mohamed Mwachausa, amesema lengo kuu la mchakato huo ni kuwaleta pamoja wadau hao na kutambua changamoto zinazokabili kesi za ugaidi nchini.
Kwa upande wake Kamishna wa kaunti ya Lamu Joseph Kanyiri, amesema visa vya itikadi hali na ugaidi vimepungua kiasi kutoka na ushirikiano wa wadau mbalimbali, japo akawasisitiza wazazi kuwapa muelekeo bora watoto wao.