Story by Hussein Mdune-
Afisa wa afya ya uzazi kaunti ya Kwale Edward Mumbo amesema visa vya mimba za mapema kwa watoto wa chini ya umri wa miaka 19 vimepungua katika kaunti hiyo.
Mumbo amesema mwaka wa 2021/2022 visa vya watoto wadogo kupachukwa mimba vilikuwa asilimia 20 lakini sasa vimepungua kutokana na juhudi za wadau mbalimbali wa kijinsia kuihamasisha jamii.
Aidha Mumbo amehoji kwamba hamasa hizo zimechangia visa hivyo kupungua kwa asilimia 17 na huenda vikakomeshwa kabisa kufikia mwaka wa 2023 iwapo juhudi hizo zitaendelezwa zaidi.
Wakati uo huo amewataka wazazi kushirikiana na Idara husika pamoja na viongozi wa kidini ili kuhakikisha watoto wanapewa elimu ya kuwajenga kimaadili.