Idara ya usalama kule Magarini kaunti ya Kilifi imedokeza kuwa visa vya watu kuuwawa kwa kukatwa mapanga kwa tuhma za uchawi vimeanza kushuhudiwa.
Afisa mkuu wa Polisi eneo hilo Gerald Barasa amesema katika siku za hivi majuzi visa kadhaa vya watu kuuawa kwa kukatwa mapanga vimeripotiwa kwenye vitongoji mbali mbali eneo hilo huku sababu kuu zikisalia kitendawili.
Barasa ameeleza kuwa idara ya usalama eneo hilo itakabiliana vilivyo na watakaohusika na mauaji hayo ya wazee.
Amesema kila mtu ana haki ya kiishi hivyo basi sio sawa kwa kuwangamiza wazee katika jamii kwa tuhma za uchawi ilhali wazee hao kamwe sio wachawi.
Taarifa na Esther Mwagandi.