Picha kwa hisani –
Idara ya usalama katika kaunti ya Kwale imesema asilimia kubwa ya visa vya dhulma za kingono vinavyoripotiwa kwa idara hio na wakaazi ni uzushi.
Kamanda wa polisi kaunti ya Kwale Joseph Nthenge amesema mara nyingi wakaazi huwasingizia watuhumiwa kwani licha ya idara hio kufanya uchunguzi juu ya visa vinavyoripotiwa hakuna ushahidi unaopatikana.
Nthenge amesema wakaazi watakaobainika kwamba wametoa ripoti za uongo kwa idara hio watachukuliwa hatua kali ikiwemo kufunguliwa mashataka.
Kauli yake inajiri baada ya mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 39 kutoka eneo la kubo ambaye ni mlemavu kushtakiwa kwa madai ya uongo ya kumnajisi mtoto wa mamake wa kambo.