Takriban visa 3,000 vya dhulma za watoto vimeripotiwa katika kaunti ya Kilifi kati ya mwezi Juni 2017 na mwezi Juni 2018.
Hii ni kulingana na ripoti iliyotolewa na shirika la kutetea haki za binadam la Haki Africa katika Chuo Kikuu cha Pwani.
Akitoa ripoti hiyo Naibu Mkurugenzi wa shirika hilo, Bi Salma Hemmed amesema kwamba ndani ya miezi mitatu visa 40 vya dhulma dhidi ya wanawake na watoto pia vimeweza kuripotiwa.
Salma ameitaja mila ya kulipia fidia kwa waathiriwa wa dhulma za kijinsia almaarufu malu kuwa chanzo kikuu katika kuendelezwa kwa visa hivyo.
Taarifa na Marieta Anzazi.