Picha kwa hisani –
Viongozi wa kisiasa humu nchini wametoa kauli zao kuhusu kuhairishwa kwa uzinduzi wa zoezi la kukusanya saini milioni moja za BBI uliopangwa kufanyika hii leo
Kinara wa ANC Musalia Mudavadi amepongeza kuhairishwa kwa uzinduzi huo akisema hatua hio itatoa nafasi ya mazungumzo zaidi kati ya wadau husika ili kuhakikisha mapendekezo ya kila mmoja yanajumuishwa kwenye ripoti hio.
Akizungumza na wanahabari mapema leo Mudavadi amesema ili taifa kuwa na amani ni lazima kuwe na mfumo wa uongozi jumuishi,akisema wakenya wanapaswa kutumia fursa hio kikamilifu kwa kuwasilisha mapendekezo yao.
Kwa upande wao viongozi wa kike katika ukanda wa pwani wakiongozwa na mwenyekiti wa makundi ya walemavu Bi Khamisa Maalim Zajjah wamewasihi wakaazi wa ukanda huu kuhakikisha wanaielewa ripoti hio kabla ya kutia saini.